Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kutoa mafunzo kwa wahamiaji wa Afrika walioko ughaibuni

IOM kutoa mafunzo kwa wahamiaji wa Afrika walioko ughaibuni

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, liko katika mpango maalum unaolenga kutoa mafunzo kwa wahamiaji wa Afrika wanaoishi ughaibuni ili wasaidie maendeleo katika nchi zao kulingana na ujuzi walionao.

Katika mahojiano na mwandishi wetu Joseph Msami msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe anasema mpango huo utahimizwa katika nchi mbalimbali baada ya kuonekana una mafanikio na hivi sasa IOM inaanza kwa wahamiaji wa Somalia walioko nchini Uingereza na kisha kuhusisha nchi nyingine barani Afrika ambazo zimeathiriwa na migogoro na zinazothamini vipaji vya raia wao walioko nje.

(SAUTI –MAHOJIANO NA JUMBE)