UNICEF yahofia watoto kukosa chanjo

19 Aprili 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lina wasiwasi kuwa matarajio ya watoto wote duniani kupata chanjo muhimu yanaweza kutumbukia nyongo kutokana na baadhi ya nchi kutotenga bajeti za kampeni hiyokamaanavyoripoti Joshua Mmali.

(TAARIFA JOSHUA)

UNICEF inaingia hofu hiyo kwa kuwa takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2011 watoto Milioni Moja na Nusu duniani wasingalifariki dunia iwapo wangalikuwa wamepatiwa chanjo za msingi dhidi ya magonjwa hatari.

UNICEF inasema mtoto mmoja kati ya watoto watano hapati chanjo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo uhaba wa fedha na mizozo ambapo wametajaSyriana Afrika Magharibi.

Hata hivyo imesema mtoto akipata chanjo kunapunguza gharama za zitokanazo na tiba iwapo atakosa chanjo hiyo. Hata hivyo UNICEF imeingia wasiwasi kwa kuwa mwaka 2011 ni nchi 152 tu kati ya 193 wanachama wa WHO ambazo zilitenga bajeti maalum kwa ajili ya chanjo.