Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wapongeza kuanza kwa upigaji kura Iraq kwa amani

UM wapongeza kuanza kwa upigaji kura Iraq kwa amani

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Martin Kobler ameelezea kuridhishwa kwake na kuanza kwa zoezi maalum la upigaji kura kuchagua magavana wa mabaraza nchini humo ambapo askari na polisi wamejitokeza kupiga kura kabla ya wananchi wengine kufanya hivyo wiki ijayo.Martin Kobler amesema hatua hiyo imefungua njia kuashiria kufanyika kwa uchaguzi kwa amani ambao unatazamiwa kufungua ukurasa wa ukomavu wa kidemokrasia.

Makundi maalumu ikiwemo askari wameanza kupiga kura na baadaye kutafuatiwa na zoezi jumla ya litakalofanyika April 20.

Zaidi ya watu milioni 15 wamejiandikisha kupiga kura katika uchaguzi ambao umewavutia wagombea 8,000 wanaowania nafasi 378.