Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama laitaka serikali ya Sudan Kusini kuchunguza mauaji ya walinda amani

Baraza la Usalama laitaka serikali ya Sudan Kusini kuchunguza mauaji ya walinda amani

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia limetoa taarifa ya kulaani vikali shambulizi la Aprili 9 asubuhi, lililowaua walinda amani watano na wafanyakazi wengine wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa Sudan Kusini, UNMISS, na kutoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kuchunguza haraka tukio hilo, na kuwawajibisha wahalifu kisheria.

Wanachama wa Baraza hilo wametuma risala za rambirambi kwa familia za walinda amani hao, pamoja na serikali ya India.

Baraza hilo limetoa ahadi ya kuunga mkono ujumbe wa UNMISS na nchi zinazochangia vikosi kwenye ujumbe huo, na kutoa wito kwa makundi yote nchini Sudan Kusini kushirikiana na UNMISS.