Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM walaani mashambulizi ya kupangwa Iraq

UM walaani mashambulizi ya kupangwa Iraq

Nchini Iraq mashambulizi ya kuvizia yameendelea kutokea na kusababisha vifo na majeruhi ambapo Umoja wa Mataifa umetoa kauli kamaanavyoripoti George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE)

Maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq wameshutumu vikali tukio la mashambulizi ya kupangwa yaliyotekelezwa Mjini Baghadad na eneo la kaskazini mwa mji waKirkukambako watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa.

Katika taarifa ya kulaani mashambulizi hayo, Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq Martin Kobler, amefananisha matukio hayo kama ni unyama unaochukiza.

Amesema kuwa matukio hayo siyo tu kwamba yanachukiza na kubeba sura ya ukatili wa hali ya juu, lakini yanajaribu kufifisha sura ya matumaini na amani ambayo wananchi wa taifa hilo wanaanza kujivunia.

Hata hivyo amesema kuwa vitendo hivyo haviwezi kuvunja moyo wananchi wa Iraq ambao sasa wanachukua mkondo mpya wa ujenzi wa amani na maridhia