Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban ziarani Ulaya Jumamosi

Ban ziarani Ulaya Jumamosi

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon anatarajiwa kuondokaNew yorkjumamosi hii  kuzuru nchi tano barani Ulaya ambako atazungumzia malengo ya maendeleo ya millennia (MDGS), silaha za kemikali na mahakama za UM

Ziara hiyo inajumuisha nchi tano ikiwemoSan Marino,Andorra,Monaco,Uhollanzi na Uhispania atakapo zindua kubakia kwa siku 1000 kufikia kilele cha utekelezaji wa Malengo ya millennia .

Malengo ya millennia ya mwaka 2000 yako manane ambayo ni pamoja na Kutokomeza umaskini, kuboresha  elimu, kuweka usawa wa kijinsia, na kuimarisha afya ya uzazi.