Maiti zaidi ya 20 wabainika huko Yemen, IOM yatoa ombi

26 Machi 2013

Sintofahamu imelikumba shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM baada ya taarifa za kuwepo kwa mlundikano wa maiti za watu wanaosadikiwa kuwa ni wahamiaji kwenye nyumba moja karibu na ofisi za shirika hilo kwenye mji wa Harath, Kaskazini mwa Yemeni.Taarifa hizo zinakuja wakati huu ambapo IOM inahaha kupata fedha za dharura kusaidia wahamiaji walioshindwa kuendelea na safari zao za ughaibuni.

Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM na anazungumzia taarifa hizo.

(SAUTI YA JUMBE) 35"