Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bado ugonjwa wa Kifua Kikuu ni tatizo sugu: WHO

Bado ugonjwa wa Kifua Kikuu ni tatizo sugu: WHO

Machi 24 kila mwaka,  dunia huadhimisha siku ya ugonjwa wa kifua kikuu. Makala yetu wikii hii inajikita katika maadhimisho hayo yatakayofanyika mwishoni mwa juma.

Ugunduzi rasmi wa ugonjwa wa kifua kikuu unafuatia kugunduliwa kwa bakteria wanaoambukiza ugonjwa wa kifua kikuu mnamo Mwaka 1882.

WHO linasema Ugonjwa wa kifua kikuu au kwa jina la kitaalamu TB ni ugonjwa wa pili kwa kusababisha vifo vya watu wengi duniani nyuma ya ugonjwa wa Ukimwi.  Ili kufahamu mengi juu ya maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa kifua kikuu, ungana na Joseph Msami katika makala hii.

(Makala: Kifua Kikuu)