Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto waliotoroshwa kwenda Sudan Kusini warejeshwa Uganda:IOM

Watoto waliotoroshwa kwenda Sudan Kusini warejeshwa Uganda:IOM

Shirika la kimataifa la wahamiaji, IOM limefanikisha kurejeshwa nyumbani salama nchini Uganda kwa watoto watano waliokuwa wamesafirishwa kiharamu kwenda Sudan Kusini. IOM inasema wazazi wa watoto hao wenye umri wa kati ya miaka 10 hadi 16 waliridhia watoto wao waende Sudan Kusini ili wasomeshwe lakini kinyume chake walikuwa wanatumikishwa kwa kuchuuza bidhaa ndogo ndogo barabarani. IOM imesema taarifa za watoto hao kutumikishwa zilizotolewa na wasamaria wema huko Juba, Sudan Kusini.

Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE):