Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na nchi za Caribbean zajadili usalama mipakani

IOM na nchi za Caribbean zajadili usalama mipakani

Maafisa kutoka mataifa 11 yaliyoko kwenye ukanda wa Caribbean wameanza kukutana kwa ajili ya kujadilia haja ya kuongeza mashirikiano kwa ajili ya kuimarisha hali ya usalama katika maeneo ya mipakani.  Mkutano huo wa siku mbili ambao umegharimiwa na Marekani unaratibiwa na  IOM. Pamoja na agenda ya uimarishwaji ulinzi na usalama katika maeneo ya mipakani wajumbe hao pia wanajadiliana kuhusu uwezekano wa kuongeza mashirikiano kwa shabaha hiyo hiyo moja ya ulinzi na usalama. Katika majadiliano hayo wataalamu wa IOM wanatazamia kuzingatia pia namna pande zote 11 zinavyoweza kutumia mifumo ya kisasa kuimarisha usalama kwenye maeneo ya mipakani na kuboresha mifumo ya ukaguzi wa hati za kusafiria.