WFP yakaribisha tangazo la Papa Francis la kuwajali maskini

19 Machi 2013

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limepongeza mwelekeo mpya ulioanzishwa na Papa Fransis ambaye pamoja na mambo ya imani lakini amesisitiza nia yake ya kuendelea kuwasaidia watu maskani hasa wale walioko Latin Amerika ambako ndiko alikozaliwa. Mkurugenzi Mkuu wa WFP Ertharin Cousin, amesema kuwa WFP amekaribisha hatua ya Papa huyo kuonyesha robo ya ubinadamu kwa kuwajali wale wenye matatizo na shida.  Bi Cousin amesema kuwa kanisa linalia kuwa na ushawishi mkubwa unaoweza kutumika kuchochea sera zinalenga kukabiliana na tatizo la njaa hasa katika mataifa yanayoendelea hivyo kwa kuzingatia uzito iliotolewa na Baba huyo Mtakatifu, WFP inashangilia kwa kuona kuwa sasa limepata uungwaji mkono wa kuwajali watu wenye shida.  Kila mwaka WFP husambaza huduma za chakula kwa watu zaidi ya milioni 90 wanaokabiliwa na njaa duniani kote .