Baraza la Usalama laiwekea DPRK vikwazo

7 Machi 2013

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo kwa kauli moja limepitisha azimio nambari 2094 la mwaka 2013, likilaani vikali jaribio la nyuklia lililotekelezwa na Jamhuri ya Korea Kaskazini,  DPRK tarehe 12 Februari, na kuiwekea upya vikwazo vikali, chini ya aya ya saba ya Mkataba Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Halikadhalika azimio hilo linaiwekea DPRK vikwazo vya kifedha, ambalo litahitaji nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhakikisha taifa hilo haliwezi kutuma au kupeleka fedha kulipia vifaa vya kutengeneza zana zake za kinyuklia.

Azimio hilo pia limewawekea vikwazo vya kusafiri maafisa wa Korea Kaskazini ambao wanahusika na biashara ya vifaa vya kinyuklia au kueneza teknolojia ya zana za kinyuklia pamoja na vikwazo vya kuzuia bidhaa za anasa kwa DPRK.  Akiongea na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kupitishwa azimio hilo, Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa, Susan Rice, amesema vikwazo hivyo vitaumiza Korea Kaskazini

(SAUTI RICE)