Uwiano ndio utaharakisha watu kurudi makwao nchini Mali: UNHCR

1 Machi 2013

Miezi miwili tangu wanajeshi wa Ufaransa waingie nchiniMalishirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linaendelea kushuhudia idadi kubwa ya wakimbizi wa ndani hasa kwenye nchi majirani.

Kati ya watu 430,000 wanaokadiriwa kulazimika kuhama makwao idadi iliyoripotiwa hadi sasa ni watu 260,665. Idadi ya wakimbizi walio nchi zaMauritania,Burkina Faso,NigernaAlgeriani watu 170,300.

Idadi ya wakimbizi wa ndani wanaorejea nyumbani bado ni ya chini hata baada ya kurejea kwa huduma za usafiri kwa njia ya barabara kati ya miji wa Bamako na Gao huku pia kukiwa a huduma za safari kwa njia ya mashua kati ya mji wa Mopti na Timbuktu. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud