Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aisifu ripoti ya ukatili dhidi ya wanawake India

Pillay aisifu ripoti ya ukatili dhidi ya wanawake India

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amekaribisha ripoti ya Kamati ya Verma kama msingi wa kuchukua hatua kukabiliana na ukatili dhidi ya wanawake nchini India, na kutoa wito kwa serikali ya India kutekeleza mapendekezo ya ripoti hiyo.

Bi Pillay ameipongeza kamati hiyo kwa kuichapisha ripoti hiyo ya kina haraka, na kwa kuyahusisha makundi ya wanawake na umma katika harakati nzima.

Amesema ripoti hiyo na mapendekezo yake ambayo ni muhimu sana, siyo tu heshima kwa msichana ambaye alibakwa na kuawa mwezi Disemba, lakini pia kwa waathirika wa ukatili wa ngono nchini India, na ishara kuwa vijana na mashirika ya umma yamejitolea kwa dhati kusema, wameona ya kutosha. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(TAARIFA YA ALICE KARIUKI)