Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya vifo vya mateka Algeria yapanda hadi 57

Idadi ya vifo vya mateka Algeria yapanda hadi 57

Idadi ya watu walio fariki dunia kufuatia tukio la siku nne la utekaji nyara katika kiwanda cha gesi cha Amenas nchini Algeria imepanda na kufika 57. Yapata watu 9 raia wa Japan wameripotiwa kuuawa, huku miili ya watu wengine 25 waliokuwa wametekwa nyara ikigunduliwa na vikosi vya Algeria.

Awali mwishoni mwa wiki, Baraza la Usalama lililaani vikali shambulio hilo la kigaidi, huku wanachama wa Baraza hilo wakielezea masikitiko na rambi rambi zao kwa jamaa za waathiriwa na serikali ya Algeria na nchi zingine ambazo raia wao waliathirika.