Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wa Mali; Umoja wa Afrika wapaza sauti

Mzozo wa Mali; Umoja wa Afrika wapaza sauti

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Rais Boni Yayi wa Benin ametaka Jumuiya ya kimataifa kuunga mkono jitihada za kuwafurusha vikundi vya wanamgambo vyenye silaha huko Mali, operesheni ambayo kwa sasa inaongozwa na Ufaransa.

Rais Yayi amesema hayo mjini Dar Es Salaam baada ya mazungumzo yake na Rais Jakaya Kikwete ambapo amesema kitendo cha waasi hao huko Mali ni tishio kwa nchi za Magharibi. Tayari Baraza la Usalama limeunga mkono operesheni hiyo ambayo imesema imezingatia mazingira tete ya mgogoro huo. George Njogopa na taarifa zaidi.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)