Tunisia iangalie upya usawa wa jinsia: Wataalamu UM

14 Januari 2013

Jopo la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa wanawake kwa misingi ya sheria na vitendo limetaka serikali ya Tunisia kuridhia vipengele vya msingi vya katiba juu ya usawa wa jinsia na kutekeleza hatua maalum za muda zitakazoharakisha ushiriki wa wanawake katika Nyanja zote za maisha.

Akizungumza mwishoni mwa ziara ya wataalam hao huko Tunisia, Kamala Chandrakirana anayeongoza kundi hilo amesema wana wasiwasi wa kuwepo kwa mianya na utata kwenye rasimu ya sasa ya katiba ambayo iwapo haitatolewa inaweza kudumaza haki za wanawake na misingi ya usawa wa kijinsia. Maelezo zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter