Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bachelet kutembelea nchi tatu za Afrika Magharibi

Bachelet kutembelea nchi tatu za Afrika Magharibi

Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-WOMEN Michelle Bachelet, atasisitiza umuhimu wa kuongeza ushiriki wa wanawake kama msingi wa kujenga taifa na maendeleo ya kiuchumi, wakati wa ziara yake Afrika Magharibiki.

Wakati wa ziara hiyo inayoanza leo hadi tarehe 11 mwezi huu, Bi Bachelet atatembelea sehemu zilio na miradi inayoipa kipaumbele uwezeshaji na haki ya wanawake katika mambo ya kiuchumi, na pia atakutana na wakuu wa nchi na maafisa wengine wa serikali na wa kiraia kwenye nchi hizo tatu akianzia Senegal, kisha Mali na hatimaye Nigeria. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)