Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada zaidi yahitajika Afghanistan

Misaada zaidi yahitajika Afghanistan

Hali mbaya ya usalama na kudorora kwa hali ya kibinadamu huenda vikaikumba Afghanistan mwaka huu wa 2013, yamesema mashirika ya kutoa misaada. 

Mpango mpya wa kibinadamu wa mwaka 2013 uliochapishwa na Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA unasema kuwa kufuatia kuzoroteka kwa hali katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ni ishara kwamba raia wataendelea kuteseka kutokana na ghasia huku hali ya kibinadamu ikidorora zadi. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)