Skip to main content

Sijasema Assad atakaa madarakani hadi 2014: Brahimi

Sijasema Assad atakaa madarakani hadi 2014: Brahimi

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu katika mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi Jumamosi atakuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, mjini Mosciw, ikiwa ni katika jitihada za kupatia suluhu mgogoro wa Syria.

Taarifa hizo ni kwa mujib uwa msemaji wa Umoja wa Mataifa, taarifa iliyotolewa Ijumaa.

Halikadhali msemaji huyo ametumia fursa hiyo kufafanua kauli ya Bwana Brahimi kuhusu serikali ya mpito nchini Syria. Amesema kamwe Brahimi hajasema kuwa Rais Bashar Al-Assad wa Syria atakuwepo madarakani hadi mwaka 2014.

Badala yake ameeleza kuwa mjumbe huyo amekuwa akirejelea mara kwa mara ya kwamba kipindi cha mpito kinapaswa kuanza mara moja na kwamba serikali inapaswa kuanzisha punde tu.

Amesema ni matumaini yake kuwa mgogoro utakuwa umepatiwa suluhu mwaka 2013 kwa kuwa haiwezi kusubiri hadi mwaka 2014.