ICTR yamhukumu Waziri wa zamani wa Rwanda kifungo cha miaka 35 jela

20 Disemba 2012

Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Rwanda, imemhukumu waziri wa zamani wa nchi hiyo Augustin Ngirabatware kifungo cha miaka 35 jela baada ya kumpata na hatia ya kuhusika na mauaji ya halaiki nchini mwake mwaka 1994.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji William Hussein aliyeongoza jopo la majaji watatu amesema Ngirabatware amepatikana na hatia ya kuhusika na mauaji, kuchochea wapiganaji wake kutekeleza mauaji ya halaiki, ubakaji na ukatili dhidi ya binadamu.

Ngirabatware ambaye wakati wa mauaji hayo alikuwa waziri wa mipango alikamatwa mwaka 2007 nchini Ujerumani na kupelekwa Arusha, Tanzania kwenye mahakama hiyo.

Takribani watu Laki Nane wengi wao watusi na wahutu wa mrengo wa kati waliuawa katika siku 100 za mauaji hayo nchini Rwanda.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter