Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 55 wafa maji huko Somalia: UNHCR

Watu 55 wafa maji huko Somalia: UNHCR

Watu hamsini na watano wakiwemo raia wa Somalia na Ethiopia wanahofiwa kufa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama kando mwa pwani ya Somalia siku ya Jumanne.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema maiti 23 wamepatikana na watu wengine 32 bado hawajulikani walipo kwa hiyo inaaminika wamezama.

Watu hao walikuwa wakisafiri kwa boti iliyokuwa imebeba watu wengi kuliko idadi yake na ilizama robo saa baada ya kuondoka bandari ya Bosasso kwenye jimbo la Puntland la Somalia lililojitangazia uhuru.