Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo dhahiri yamepatikana katika ujenzi wa amani: Ban

Maendeleo dhahiri yamepatikana katika ujenzi wa amani: Ban

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu ujenzi wa amani baada ya migogoro ambapo Katibu Mkuu Ban Ki- Moon amesema maendeleo ya dhati yamepatikana katika ajenda ya ujenzi wa amani.

Akihutubia kikao hicho, Bwana Ban amesema hata licha ya mafanikio yaliyopatikana, bado kuna changamoto lukuki.

Amesema baadhi ya nchi bado zimeendelea kukumbwa na ukosefu wa utulivu hata baada ya kumalizika kwa migogoro, na kuwa na uwezekano mkubwa wa kutumbukia tena kwenye ghasia.

Mathalani Bwana Ban amesema asilimia 90 ya migogoro ya kati ya mwaka 2000 na 2009 ilitokea kwenye nchi ambazo awali zilikumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

(SAUTI YA BAN)