Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wengi wayakimbia machafuko Misri, UNRWA yakabiliwa na mzigo wa wakimbizi wa ndani

Wengi wayakimbia machafuko Misri, UNRWA yakabiliwa na mzigo wa wakimbizi wa ndani

Kumekuwa na hali ya mkwamo unaowaandama raia wa Syria katika wakati ambapo matokeo ya mzozo huo umeathiri pia ustawi jumla ya wale wanaotajwa wakimbizi wa Kipalestina.

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi wa Palestina UNRWA, limeanzisha juhudi ya usambazaji wa huduma za kibinadamu kwa zaidi ya wakimbizi 150,000 walioko katika kambi ya Yarmouk.

Hali pia ni ya mashaka kwa raia wengine wa Syria ambao baadhi yao wanalazimika kwenda uhamishoni kutokana na kuchacha kwa mapigano hayo.

Ripoti zinasema kuwa idadi ya wakimbizi walioko kwenye kambo ya Yarmouk inazidi kuongezeka katika wakati huduma za dhararu zikipatikana kwa shida,

UNRWA imetoa hifadhi kwa zaidi ya watu 2,600 ambao wamekosa makazi baada ya kukimbia machafuko mjini Damascus na kuna uwezekano idadi hiyo ikaongezeka zaidi katika siku za usoni.