Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siku ya kimataifa ya haki za binadamu

Siku ya kimataifa ya haki za binadamu

Sauti yangu ina nafasi! Ni ujumbe wa siku ya kimataifa ya haki za binadamu iliyoadhimishwa tarehe 10 Desemba mwaka huu, siku ambayo miaka 64 iliyopita lilipitishwa tamko la kimataifa la haki za kibinadamu.

Mwaka huu ujumbe huo unatoa fursa kwa makundi yote hususan wanawake, vijana, makundi madogo, walemavu, wapenzi wa jinsia moja, mashoga na hata wale waliobadili jinsia zao kupaza sauti zao ili ziweze kusikika na haki zao kuzingatiwa. Katika makala ya wiki hii, Assumpta Massoi ameangazia jinsi Umoja wa Mataifa ulivyoadhimisha siku hiyo kwa lengo la kutetea haki za makundi yote.