Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taratibu za kuwafikisha watuhumiwa wa uhalifu Darfur zaendelea: Bensouda

Taratibu za kuwafikisha watuhumiwa wa uhalifu Darfur zaendelea: Bensouda

Baraza la Usalama hii leo limepokea ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki Moon kuhusu Sudan ambayo pamoja na mambo mengine imeelezea hatua zilizofikiwa katika kuwafikisha mbele ya sheria watuhumiwa vitendo vya uhalifu huko Darfur.

Ripoti hiyo imewasilishwa na mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, Fatou Bensouda ambaye amesema tayari wamepatikana watuhumiwa watano ambao mashtaka yao yamepangwa kuanza kusikilizwa mwakani.

Hata hivyo amesema kuwa upande wa utetezi umeomba kesi hiyo kusogezwa mbele kwa sababu mbali mbali ikiwemo tafsiri ya nyaraka kwa lugha ambayo inatumiwa na watuhumiwa ili haki iweze kutendeka.