Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama lasikitishwa na kitendo cha DPRK: Kuchukua hatua iwapo itakiuka tena azimio

Baraza la Usalama lasikitishwa na kitendo cha DPRK: Kuchukua hatua iwapo itakiuka tena azimio

Wajumbe wa Baraza la Usalama leo wamefanya mashauriano kuhusu hofu na wasiwasi ulioibuka kufuatia kitendo cha Jumanne cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK kurusha roketi kwa kutumia teknolojia ya makombora ya masafa marefu ambapo wameshutumu vikali kitendo hicho.

Rais wa Baraza hilo Mohammed Loulichki amewaambia waandishi wa habari baada ya mashauriano hayo kuwa kitendo hicho ni kinyume cha azimio namba 1874 la mwaka huu la Baraza hilo dhidi ya DPRK.

(SAUTI Loulichki)