Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi bado wanahitaji msaada ukanda wa Gaza: OCHA

Watu zaidi bado wanahitaji msaada ukanda wa Gaza: OCHA

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Kundi la Hamas chini ya uongozi wa Misri yaliyoanza kutekelezwa tarehe 21 mwezi Novemba yamewafanya wapalestina wengi kuyafikia maeneo ya uvuvi na kilimo ambayo awali hawakuwa wakiyafikia.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa kulingana na ya tathmini iliyoendeshwa ni kwamba bado watu 3000 wamehama makwao kutokana na kuharibiwa kwa makwao. Baadhi ya changamoto zilizopo kwa sasa ni ukarabati wa makao yaliyoharibiwa pamoja na shule na kuwapa msaada wa kisaikolojia watoto.

OCHA inasema kuwa fedha zinazohitajika kugharamia mahitaji kutokana na ghasia zilizoshuhudiwa mwaka 2012 zinakadiriwa kuwa kati ya dola milioni 60 na milioni 70.