Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ombi la dola bilioni 1.3 kwa miradi ya kibinadamu lazinduliwa Somalia

Ombi la dola bilioni 1.3 kwa miradi ya kibinadamu lazinduliwa Somalia

Ombi la miaka mitatu kwa taifa la Somalia limezinduliwa humo ikiwa ndiyo mara ya kwanza uzinduzi huo kufanyika nchini Somalia. Ombi hili liliwasilishwa na naibu mratibu wa huduma za kibinadamu nchini Somalia Stefano Porretti kwa Waziri wa usalama na masuala ya ndani nchini Somalia Abdikarim Hussein Guled anayehusika na masuala ya kibinadamu.

Mkakati huo kati ya mwaka 2013-2015 unalenga mahitaji ya kibinadamu kwa watu wa Somalia. Jens Laerke ambaye ni msemaji wa Shirika la kuratibu masusla ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA mjini Geneva anaeleza kuhusu ombi hilo.

"Kwa mwaka ujao  tunaomba  dola Milioni Moja nukta Tatu kusaidia kutekeleza programu za misaada ya kibinadamu tuliyopanga kuwafikia na kuwasaidia wasomali 3.8 milioni walioko ndani ya nchi hiyo.  Na bado kunaendelea kuwepo kwa mahitaji ya haraka ya kibinadamu, pia tunaangalia programu kwa ajili ya kujenga mazingira ya kukabiliana na matatizo kwa manufaa ya baadaye  ili pengine tuunaweza  kuondokana na mzunguko huu wa matatizo wa miaka 20 ulioshuhudia matatizo ya mara kwa mara kama vile migogoro, mapigano, njaa, ukame na kadhalika".