UNHCR yaelezea wasi wasi wake kuhusu usalama wa watu kwenye kambi mashariki mwa DRC

4 Disemba 2012

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa linahofia usalama wa watu waliohama makwao pamoja na watoa huduma za misaada kwenye kambi zilizo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya shambulizi nje ya kambi ya Mugunga III iliyo mjini Goma siku ya Jumamosi. Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anasema kuwa hata hivyo anasema kuwa hakukuwa na vifo wala majeruhi lakini mtu mmoja alipigwa vibaya huku nyumba na duka la dawa vikiporwa.

(SAUTI YA ADRIAN EDWARDS)

Kulingana na tathmini iliyofanywa na UNICEF na washirika wake miongoni mwa familia zilizohama mwakao mjini Goma na Sake ni kuwa kuna muhaba mkubwa wa mahitaji ikiwemo mitungi ya ya maji, neti za mbu, vyombo vya kupikia na nguo. Takriban visa 12 vya dhuluma za kimapenzi vimneripotiwa kwenye kambi ya Kungunga.