Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wazindua kampeni ya kupiga vita vitendo vya unyanyapaa sehemu ya kazi

UM wazindua kampeni ya kupiga vita vitendo vya unyanyapaa sehemu ya kazi

Wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wamezindua kampeni yenye shabaha ya kulinda na kutetea haki za watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi ambao wanaandamwa na vitendo vya unyanyapaa wawapa kwenye maeneo yao ka kazi.

Mkuu wa shirika la kazi ulimwenguni ILO Guy Ryder amesema kuwa kupiga vita vitendo vya unyanyapaa kwenye maene ya kazi ni jambo muhimu na tena lisilokwepeka hasa wakati huu wa kuendeleza mapambano ya maambukizi mapya ya HIV.

Amesema dunia inaweza kufaulu kushibda kuenea kwa maambukizi ya HIV kwa kushikamana pamona na kupinga vitendo vya unyanyapaa kwenye maeneo ya kazi.

Vitendo vya unyanyapaa vinaelezwa kuwaandama zaidi ya watu milioni 30 ambao wamefikia umri wa kufanya kazi lakini wanakoseshwa fursa hizo kutokana na kuishi na virusi vya HIV. Taarifa kamili na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)