Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP yaongoza jitihada za kudhibiti kemikali zenye sumu

UNDP yaongoza jitihada za kudhibiti kemikali zenye sumu

Umoja wa Mataifa unasema kuwa wakazi wa nchi zinazoendelea wako katika hatari kubwa zaidi ya kupata madhara yatokanayo na kemikali hatari ambazo hutelekezwa hovyo bila kujali madhara kwa binadamu.

Harakati za kupunguza madhara ya kemikali za sumu hasa kwa nchi hizo maskini zinaendelea kuimarishwa katika mikutano mbali mbali ikiwemo unaomalizika leo mjini New York , Marekani.

Mkutano huo wa 38 wa programu ya pamoja ya kudhibiti vyema kemikali, IOMC unaangalia hatua zinazofuatia mkutano wa RIO+20 ambapo mataifa mbali mbali yalikubaliana kuwa ifikapo mwaka 2020 wafikie lengo la kushughulikia vyema kemikali za sumu ili wakati wote zinapotumiwa hadi kuteketezwa zisiwe na madhara kwa maisha ya binadamu. Taarifa zaidi na Monica Morara: