Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waomba dola milioni 41 zaidi kwa mahitaji yaloongezeka jimbo la Rakhine Myanmar

UM waomba dola milioni 41 zaidi kwa mahitaji yaloongezeka jimbo la Rakhine Myanmar

Mratibu wa masuala ya misaada ya kibinadamu nchini Myanmar, Ashok Nigam, leo amezindua mpango mpya wa kuitikia mahitaji ya dharura ya kibinadamu katika jimbo la Rakhine, Myanmar.

Wakati wa uzinduzi huo, Bwana Nigam, ambaye aliandamana na waziri wa masuala ya mipaka Myanmar, Jenerali Thein Htay, ameishukuru jamii ya kimataifa kwa mchango wake kufikia sasa, na kuomba iendelee kutoa msaada huo.

Mpango huo mypa utatoa misaada ya dharura kwa watu laki moja na kumi na tano elfu, ambao wamelazimika kuhama makwao kutokana na vita vya kijamii katika jimbo la Rakhine, kufikia Juni mwaka 2013. George Njogopa na taarifa kamili

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)