Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya kutoa misaada yakabiliana na athari za kimbunga Sandy nchini Haiti

Mashirika ya kutoa misaada yakabiliana na athari za kimbunga Sandy nchini Haiti

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA linasema kuwa kimbunga Sandy kinaripotiwa kuwaua watu 60 nchini Haiti na kuwaathiri wengine milioni 1.8 ambapo pia nyumba 18,000 ziliharibiwa.

Kwa upande wake shirika la afya duniani WHO linasema kuwa hali mbaya ya usafi nchini Haiti huenda ikachangia kuwepo kwa magonjwa ya kuambukiza ukiwemo ugonjwa wa kipindupindu. Hata hivyo vituo 22 vya kutibu ugonjwa wa kipindupindu viliharibiwa na kimbunga hicho.

Nalo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linasema kuwa mvua iliyosababishwa na kimbunga Sandy nchini Haiti ilisababisha mafuriko na kulaumiwa kwa visa vya ugonjwa wa kipindupindu na kwa vifo vya watu watatu kwenye mji wa Gonaives. Kati ya visa 277 vya ugonjwa wa kipindupindu vilivyoripotiwa 117 viko kwenye mjii mkuuu Port-au-Prince. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMAR JUMBE)

Nako nchini Cuba zaidi ya watu 500,000 waliathiriwa kwemye mji wa pili kwa ukubwa ambapo zaidi ya watu 190,000 walipatwa matatizo ya umeme.