Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mafuriko makubwa yaikumba Nigeria

Mafuriko makubwa yaikumba Nigeria

Karibu watu milioni 1.3 nchini Nigeria wamelazimika kuhama makwao huku wengine 431 wakiwa wameaga dunia kufuatia mafuriko ambayo yanatajwa na serikali kuwa mabaya zaidi kuwai kushuhudiwa kwa kipindi cha miaka 40 iliyopita.

Kulingana na halmashauri ya kitaifa inayohusika na majanga ya dharura NEMA, Majimbo 30 kati ya majimbo 36 yameathiriwa tangu mwezi Julai. Kufuatia mvua kubwa, majimbo ya Delta na Bayelsa yamefurika na kuathiri jamii 350 ambapo watu 120,000 waliachwa bila makao. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)