Waziri Mkuu wa zamani wa Italia ateuliwa mjumbe wa UM Sahel

9 Oktoba 2012

Waziri Mkuu wa zamani wa Italia, Romano Prodi ameteuliwa kuwa mjumbe maalum wa Katibu Mkuu uwa Umoja wa Mataifa huko Sahel, barani Afrika.

Martin Nesirky ambaye ni msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema Prodi ataongoza harakati za Umoja wa Mataifa na kimataifa katika kupatia suluhu matatizo yanayokumba watu wa eneo la Sahel na nchi za Afrika Kaskazini kuanzia bahari ya Sham hadi zile zinazopakana na bahari ya Atlantiki, matatizo kama vile uchumi usio tulivu, hali mbaya ya hewa na mizozo.

"Mjumbe huyo maalum atatekeleza majukumu yake kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, hususan kusaidia juhudi za kitaifa, kikanda na kimataifa juu ya masuala yahusianayo na mipaka na baina ya nchi. Atasaidia kuchochea, kuendeleza na kuratibu ushiriki wa kimataifa katika kujenga utaifa wa nchi za eneo la Sahel ikiwemo migogoro yenye sura nyingi akianzia na Mali.”

===

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter