UM wakaribisha tangazo la serikali ya Afghanistan kuhusu mwanamke “kukimbia”

4 Oktoba 2012

Umoja wa Mataifa umesema kuwa umefurahishwa na taarifa iliyotolewa hadharani na serikali ya Afghanistan iliyosema kuwa siyo kosa la. jinai kwa mwanamke ama mtoto wa kike kukimbia kutoka eneo lake hasa pale anapoandamwa na jambo ambalo linaweza kudhuru afya yake.

Hivi karibuni mawaziri kadhaa walitoa tamko la kulaani vikali tukio la kutiwa mbaroni wanawake na wasiachana kadhaa ambao wanadaiwa kukimbia mbio.Waendesha mashtaka nchini humo wanatumia , tukio la mwanamke kukimbia kama sehemu ya ushahidi wao muhimu wa kumtia hatiani mwanamke kuwa alikuwa na mipango ya kutenda zinai, tendo ambalo ni uhalifu chini ya sheria ya kiislamu yaani sharia.

Katika taarifa yake Umoja wa Mataifa pamoja na kupongeza hatua ya mawaziri hao lakini imesisitiza haja ya kuwepo mipaka ili kuhakisha kwamba hakuna mamlaka inayolazimisha utekelezwaji wa sheria inayomnyima mtu uhuru wa kukimbia.

Umoja huo wa Mataifa umeongeza kusema kuwa, chini ya sheria za Afghanistan kwa mtu kikimbia siyo kosa la jinai, hivyo ni muhimu mamlaka zinazosimamia maamuzi kujiepusha na vitendo hivyo ilivyoviita vya ukandamizaji dhidi ya wanawake.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter