Sudan Kusin imefaulu mtihani ndani ya mwaka mmoja, asema Makamu wa Rais

28 Septemba 2012

Akizungumza kwenye baraza kuu la Umoja wa Mataifa, Makamu wa rais wa Sudan Kusin Riek Machar amewaambia wajumbe kwenye kongamano hilo kuwa pamoja na mikwamo inayoendelea kuikabali taifa hulo, lakini katika uhai wake wa mwaka moja Sudan Kusin imefafanua kuwa ni taifa liloweza.

Amesema taifa change lililozaliwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, limejaribiwa na kufuza mtihani kuwa linaweza na kinachosalia sasa ni kuendelea kuungwa mkono toka jumuiya ya kimataifa.

Sudan Kusin ilikuwa taifa jipya na huru tahehe 9 July , mwaka 2011. Kuzaliwa upya kwa taifa hilo ni matokeo ya utekelezwaji wa mpango wa usitishwaji mapigano yaliyodumu kwa zaidi ya miaka 6 na kuvuruga ustawi wa eneo hilo.

Hata hivyo kumekuwa na hali ya mvutano baina ya pande mbili Sudan Kusin na Sudan kila upande ukigombea eneo linalotajwa kuwa na rasilimali za mafuta. Pande hozo mbili hapo majuzi zilitiliana saini makubaliano yanayopisha hali ya mashaka mashaka.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter