Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano kuhusu dhuluma za kimapenzi kwenye mizozo waandaliwa New York

Mkutano kuhusu dhuluma za kimapenzi kwenye mizozo waandaliwa New York

Waziri wa mambo ya kigeni wa uingereza, kitengo cha wanawake wa Umoja wa Mataifa UN WOMEN , Ofisi maalum ya katibu mkuu kuhusu dhuluma za kimapenzi kwenye mizozo na kampeni ya kimataifa ya kukomesha ubakaji na dhuluma za kijinsia wanatoa wito kwa viongozi kuchukua hatua madhubuti ili kuwahakikishia haki waathiriwa wa mizozo inayohusiana na dhuluma za kimapenzi na dhuluma za kijinsia.

Wakiwa mjini New York waziri wa mambo ya kigeni wa uingereza William Hague, mkurugenzi wa kundi la wanawake wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet , mjumbe maalum wa katibu mkuu kwenye masuala ya dhuluma za kimapenzi kwenye mizozo Zainabu Bangura pamoja na mshindi wa tuzo la amani Leymah Gbowee wanatarajiwa kuhutubia kikao ambacho kitahudhuriwa nchi wanachama, mashirika ya Umoja wa Mataifa na zaidi ya mashirika 30 yasiyokuwa ya kiserikali. Kwenye sehemu za mizozo wanawake huwa wanaathiriwa zaidi na dhuluma na kimapenzi na za kijinsia, uhamiaji wa lazima na ukiukaji wa haki za binadamu.