Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban awasihi viongozi wa kimataifa kuitikia matakwa ya watu wao sasa

Ban awasihi viongozi wa kimataifa kuitikia matakwa ya watu wao sasa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, ametoa wito kwa viongozi wote duniani kuzingatia mahitaji muhimu ya watu wanaowaongoza, ili kuhakikisha wanaona maendeleo katika maisha yao sasa, bila kuchelewa.

Bwana Ban amesema hayo katika hotuba yake ya kufungua rasmi mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambao unaendelea sasa katika makao makuu mjini New York. Katibu Mkuu, ambaye ameitaja hotuba yake kama mbiu ya mgambo kwa wanadamu, amesema ulimwengu unakabiliwa kwa kiasi kikubwa na ukosefu wa usalama, kutokuwepo usawa na kutovumiliana.

Amesema serikali nyingi zinafuja mali muhimu kwa kununua silaha kali, huku zikipunguza uwekezaji katika watu, akisisitiza kwamba watu wanataka ajira na matumaini ya maisha bora. Badala yake, Bwana Ban amesema, wanachopata mara nyingi huwa ni migawanyiko, kucheleweshwa na kunyimwa nafasi ya kuona ndoto zao zikitimia. Ameongeza kuwa kuna hatua ambazo zimepigwa, hasa katika kuweka uongozi wa kidemokrasia katika mataifa ya Waarabu na kupunguza umaskini, lakini bado kuna mengi zaidi ya kufanya.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)