Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Pillay aitaka Algeria kutozibinya taasisi za kiraia

Pillay aitaka Algeria kutozibinya taasisi za kiraia

Mkuu wa kamishna ya haki za binadamu ameitaka serikali ya Algeria kuutafakari upya uamuzi wake wa kuongeza mbinyo kwa mashirika ya kiraia na akitaka uhuru zaidi kwa mashirika hayo

Akikamilisha ziara yake ya siku tatu iliyomchukua kwenye maeneo muhimu, Navi Pillay amesema ustawi wa taasisi za kiraa unaondamwa na sheria kandamiza ambazo kwa ujumla wake hazito nafasi kwa taasisi hizo kuendesha shughuli zake kwa uhuru.

Amevitaka vyombo vya kidola kujiweka kando na matumizi ya nguvu, lakini ametaka kuwepo kwa daraja la maelewano baina ya pande zote huku akihimiza Algeria kutokwenda kinyume na matamko ya kimataifa yanayohimiza uhuru wa maoni.

Katika ziara yake hiyo Navi Pillay alikutana na kufanya mazungumzo na rais Abdelaziz Bouteflika pamoja na maafisa wengine kutoka idara za kimahakama na bunge.