Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM na wanazuoni wajadili njia bora za elimu ya utumwa

UM na wanazuoni wajadili njia bora za elimu ya utumwa

Wasomi kutoka kada mbalimbali duniania wamekutana kwa shabaya ya kujadiliana njia bora na sahihi itakayosaidia kufikia mwongozo wa pamoja wa utoaji elimu ya utumwa kwa vizazi vijavyo.

Mkutano huo ambao umefanyika chini ya uratibu wa Umoja wa Mataifa umeandaliwa kwa kutumia teknolojia ya mawasiliano ya mbali yaani video conference umewahusisha pia walimu na watoa elimu rika. Jumla ya wajumbe 450 wameshiriki kwenye mkutano huo ambao umeshuhudia wataalamu hao wakibadilishana uzoefu na mbinu mpya ya ufikishajiu ujumbe kwa walengwa.

Tukio hilo ni mfulululizo wa matukio mengine kadhaa yanayoratibiwa na Umoja wa Mataifa ndani ya juma hili yenye lengo la kuadhimisha siku ya kimataifa ya kuwakumbuka waathirika wa matukio ya utumwa.