Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN-HABITAT yaandaa mkutano kujadili ongezeko la watu wanaohamishwa kwa nguvu toka kwenye makazi yao

UN-HABITAT yaandaa mkutano kujadili ongezeko la watu wanaohamishwa kwa nguvu toka kwenye makazi yao

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na makazi linajiandaa kuwa na mkutano mkubwa ikiwahusisha wataalamu wa kimataifa wa makazi ambao watakuwa na shabaya ya kuangazia mtizamo wa wale wanaohamishwa kwa kulazimishwa. Mkutano huo ambao umepangwa kufanyika kuanzia Septemba 20-23 mjini Nairobi unazingatia mpango wa kimataifa ambao umeweka hadi mwaka 2025 kuwa na makazi bora naya uhakika.

Wataalama wapatao 40 kwenye mkutano huo wanatazamiwa kubadilisha ujuzi na uzoefu lakini zingatio lao likituwama kuhusiana nafasi ya UN HABIT ambayo imeweka shabaya ya kuleta mapinduzi kwenye ujenzi. Mkutano huo unafanyika katika wakati ambapo vitendo vya kuwatimua watu kutoka kwenye makazi yao vikizidi kuongezeka.