Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mawaziri wa Afrika wakutana kukubaliana kuhusu njia za kuimarisha usajili wa umma

Mawaziri wa Afrika wakutana kukubaliana kuhusu njia za kuimarisha usajili wa umma

Mawaziri kutoka nchi 46 barani Afrika wanakutana mjini Durban, Afrika Kusini, ili kujadili jinsi ya kuimarisha usajili wa umma na mifumo ya takwimu za kitaifa. Hii ni kutokana na kutambua umuhimu wa usajili bora wa umma, na mchango wake katika kuhakikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Elke Wisch, ambaye ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF katika kanda ya Afrika Mashariki na Afrika Kusini, amesema Bila kuwa na cheti cha kuzaliwa, mtoto hawezi kuwa na uenyeji kisheria. Ameongeza kuwa usajili wa watoto ni muhimu katika kuwawezesha kupata elimu, huduma za afya, pamoja na mayatima kuweza kurithi mali ya wazazi wao. Monica Morara na taarifa kamili.

(TAARIFA YA MONICA MORARA)