Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watu wanaohama Yemen kutoka pembe ya Afrika imefurutu ada:UNHCR

Idadi ya watu wanaohama Yemen kutoka pembe ya Afrika imefurutu ada:UNHCR

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, limesema idadi ya wakimbizi kutoka Pembe ya Afrika wanaoelekea Yemen kupitia Ghuba ya Adeni na Bahari ya Sham inaendelea kuzidi viwango vya awali. Katika miezi 7 ya kwanza mwaka 2012, zaidi ya watu 63, 000 walifanya safari hiyo ngumu, ikilinganishwa na watu 48, 700 wakati kama huo mwaka uliopita, ikionyesha kupanda kwa asilimia 30.

Mwaka 2011 pia ulivunja rekodi, ambako zaidi ya watu 103, 000 waliwasili Yemen kwa njia ya bahari, ikiwa ni idadi ya juu zaidi tangu mwaka 2006, wakati UNHCR ilipoanza kukusanya habari kuhusu njia barabara hiyo ya uhamiaji.

UNHCR pia inasema idadi ya raia wa Ethiopia wanaovuka mipaka kutumia huduma za wafanya magendo walioko kwenye vuko za Somalia na Djibouti. Shirika hilo linajihusisha zaidi na wale ambao wanakimbia machafuko na utesaji katika nchi zao, na kutafuta usalama katika nchi jirani kwa njia yoyote ile, hata ikiwemo mitumbwi ya wafanya magendo. George Njogopa na taarifa kamili

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)