Ban akutana na marafiki zake aliosoma nao miaka 50 iliyopita

27 Agosti 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekutana na marafiki zake aliokutana nao kwa mara ya kwanza nusu karne iliyopita mjini Washington ambao anasema kuwa ndiyo waliompa hamasa ya kuingia kwenye utumishi wa umma.

Kusanyiko hilo ambalo liliratibiwa na chama cha msalaba mwekundi cha Marekani limetoa fursa kwa pande zote mbili kubadilishana mawazo na kukumbushana haya na yale yaliyojitokeza miaka ya nyuma.

Akizungumza kwenye kusanyiko hilo, Ban alisema kuwa, “kwa hakika nimetoa hutuba nyingi sana maishani mwangu, lakini kwa leo tukio hilo ni la kusisimua na limeniacha hoyi” alisema Ban

Akiwa kijana Ban alikumbusha namna ilivyokuwa muhimu kushinda mtihani wa lugha ya kiingereza uliohusisha wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali ili kukubaliwa kuingia kwenye mpango maalumu wa kwenda kusoma nchini Marekani

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter