Ban kuzindua kongamano la vyuo vikuu Pennsylvania

Ban kuzindua kongamano la vyuo vikuu Pennsylvania

Ban Ki-moon atafanya ziara Jumatau katika chuo kikuu cha Pennsylvania katika jimbo la Philadelphia kuzindua kikao cha tano cha kongamano la wakuu wa vyuo vikuu, alisema msemaji wake.

Kongamano hilo ni mtandao wa makansela wa vyuo vikuu vya kimatifa vinavyoangazia namna ya kupatiwa ufumbuzi matatizo ya umma kwa ujumla . Vyuo vikuu 30 hivi vitashiriki katika kongamano hilo la jumatatu.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni kuwawezesha wanawake kubadili ulimwengu : Ni upi mchango wa vyuo vikuu na Umoja wa Mataifa. Washiriki watajadili changamoto kwa ujumla zilizo njiani ili kumuwezesha mwanamama na msichana .

Na nini vyuo vikuu na Umoja wa Mataifa vinaweza kufanya ili kuruhusu ushiriki kikamilifu na uongozi wa kinamama katika jamii zao na jumuiya kwa ujumla.