Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni bora kupunguza majanga kwa kuangazia mazingira:UNEP

Ni bora kupunguza majanga kwa kuangazia mazingira:UNEP

Shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP, limetaja kuangazia mazingira kama jambo muhimu katika kuweka tahadhari dhidi ya majanga, mbele ya kongamano la kimataifa kuhusu majanga.

Haja ya kukomesha mwendo wa pole katika kugeuza fikra kuhusu tahadhari na majanga kuwa vitendo, ni mojawepo ya mambo yatakayojadiliwa katika kongamano hilo la kimataifa kuhusu tahadhari na majanga, linalofanyika nchini Uswizi mwishoni mwa wiki hii.

Shirika la UNEP ndilo linalosimamia kongamano hilo la nne la IDRC Davos, ambalo hufanyika kila baada ya miaka miwili. Kongamano hilo litawaleta pamoja zaidi ya watu 1,000, wakiwemo wataalam wa tahadhari na majanga, wahudumu katika idara za majanga na maafisa wa serikali kutoka nchi 100. Alice kariuki na ripoti kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)