Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea katika Masuala ya Kibinadamu yapitisha Lengo la Kufikia watu milioni 100

Kampeni ya Siku ya Kimataifa ya Kujitolea katika Masuala ya Kibinadamu yapitisha Lengo la Kufikia watu milioni 100

Kampeni ya kimataifa lenye lengo la kuweka historia ya mitandao ya kijamii kwa kujaribu kuwafikia watu bilioni moja hapo Agosti 19 katika kusherehekea siku ya kimataifa ya masuala ya kibinadamu, imepita lengo lake la kwanza la kufikia watu milioni 100.

Kampeni hiyo imepata msukumo mkubwa kufuatia tamasha la muziki lililofanyika Ijumaa kwenye baraza Kuu la Umoja wa Msataifa na kutumbuizwa na mwanamuziki nyota Beyonce aliyeimba kibao “Iwas Here”mbele ya mashabiki 1200,watu mashuhuri, wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu na viongozi mbalimbali.

Video ya kibao hicho ambacho Beyonce na mwandishi wa nyimbo Dianne Warren, wamekitoa msaada kwa kampeni hiyo itakayozinduliwa rasmi Agosti 19 ikimchagiza kila mtu kuwa anaweza kujitolea na kinachotakiwa ni kuchukua hatua kumsaidia mwingine.