Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi zahitajika katika kuzuia Unyanyasaji wa watoto Mashariki mwa Asia na Pacific:UNICEF

Juhudi zahitajika katika kuzuia Unyanyasaji wa watoto Mashariki mwa Asia na Pacific:UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limetoa ripoti leo Jumatato inayosema unyanyasaji wa kimwili usiokubalika unasababisha madhara ya muda mrefu kwa maisha na hatima ya watoto wengi Mashariki mwa Asia na Pacific.

Ripoti hii iitwayo “Unyanyasaji wa watoto: Ushamiri, Matukio na Athari katika Mashariki mwa Asia na Pacific” ni ya kwanza ya uchambuzi wa kina wa tafiti zilizopo, uliofanywa na wataalamu na wasomi kuhusu unyanyasaji wa watoto katika kanda.

Makadirio ya matumizi mabaya ya kimwili ya watoto inatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine, na pia kutoka kwa mafunzo tofauti tofauti, lakini ripoti hii inaonyesha kwamba hata katika mazingira bora zaidi, mtoto mmoja kati ya kumi hunyanyaswa kimwili, wakati kwa mazingira mabaya watoto asilimia 30.3 wanakabiliwa na unyanyasaji. Monica Morara na taarifa kamili.

(SAUTI YA MONICA MORARA)